Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:36

Waasi wako tayari Gadhafi abaki Libya akijiuzulu


Picha ya kiongozi wa libya Moammar Gadhafi
Picha ya kiongozi wa libya Moammar Gadhafi

Waasi wasema kama Gadhafi atapenda kubaki Libya watachagua makazi yake na harakati zake zitakuwa chini ya usimamizi wa kimataifa.


Mkuu wa waasi nchini Libya amesema upinzani uko tayari kumruhusu kiongozi wa nchi hiyo Moammar Gadhafi kubaki nchini humo kama atajiuzulu na atakubali kufuata usimamizi wa kimataifa wa harakati zake.

Katika mahojiano na shirika la habari la kimataifa reuters jumapili, Mustafa Abdel Jalil amesema waasi walitoa pendekezo lao mwezi mmoja uliopita kupitia umoja wa mataifa lakini bado hawajapata jibu.

Jalil alikuwa akizungumza kutoka mji ulio mashariki mwa Libya , Benghazi ambayo ni ngome kuu ya baraza la taifa la mpito la waasi.

Jalil alisema kama Gadhafi atajiuzulu na kuamuru wanajeshi wake kuondoka katika maeneo yao anaweza kuamua kama abaki Libya au ahamie nje ya nchi.

Kiongozi huyo wa waasi amesema kama Gadhafi atapenda kubaki waasi watachagua makazi yake na harakati zake zote zitakuwa chini ya usimamizi wa kimataifa.

Bwana gadhafi ameapa kuendelea na mapigano dhidi ya waasi mpaka mwisho, ambao walianza ghasia za kupinga utawala wake wa miaka 42 mwezi februari .

Nchi zenye nguvu duniani zimeunga mkono waasi wanaompinga na kumtaka ajiuzulu na wamechangia katika mashambulizi ya NATO kwa wanajeshi wanaomuunga mkono Gadhafi kuwazuiya kushambulia raia wa Libya.

XS
SM
MD
LG