Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 12:16

Libya: Robo ya mji wa Derna kwa kiwango kikubwa wazolewa na mafuriko


Picha hii imetolewa kutoka katika mtandao wa Kijamii wa kituo cha televisheni cha al-Masar September 13 ikionyesha uharibifu uliotokea baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko kufuatia kimbunga cha Mediterranean "Daniel".
Picha hii imetolewa kutoka katika mtandao wa Kijamii wa kituo cha televisheni cha al-Masar September 13 ikionyesha uharibifu uliotokea baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko kufuatia kimbunga cha Mediterranean "Daniel".

Mji wa Derna, makazi ya watu 125,000, umeharibiwa na Kimbunga Daniel ambacho kilibomoa mabwawa katika mto unaopita ndani yake, na kuangusha majumba na robo ya mji huo kwa kiwango kikubwa kuzolewa na mafuriko.

Miili iliyokuwa imefunikwa au kuwekwa kwenye mifuko ya plastiki ilikuwa imehifadhiwa ndani na kuzunguka eneo la Hospitali ya Wahda iliyoko Derna, Jumanne (Septemba 12) wakati mkurugenzi, Mohamad al-Qabis, alisema kuwa walihesabu miili 1700 katika sehemu moja na miili 500 katika sehemu nyingine.

“Yoyote anayetambuliwa (na familia au marafiki) anazikwa. Kuna baadhi ambao hawajatambuliwa – kwa hiyo tumeanza kuchukua picha zao na kuweka namba kwa miili hiyo, na baadaye tunawazika pia,” alisema.

Mkazi mmoja, Mustafa Salem, alisema mafuriko mabaya kabisa yametokea wakati wa usiku ambapo “ watu walikuwa wamelala, hakuna aliyekuwa tayari na hali hiyo.” Katika eneo jirani naye, aliongeza kusema “waliwapoteza watu 30 hadi sasa, wanafamilia 30 wa familia moja. Hatujaweza kumpata yeyote kati yao.”

Kiasi cha watu 10,000 wametoweka na maafisa wanatarajia idadi ya vifo itaongezeka zaidi katika nchi ambayo imegawanyika na kudidimia baada zaidi ya muongo mmoja wa vita.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG