Ndege za kivita za NATO zimeshambulia kwa mabomu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli kwenye maeneo kadhaa ijumaa.
Taarifa na majeruhi bado hazijatolewa wapi palishambuliwa . Lakini kulionekana magari mengi ya uokozi yakiwa katika mitaa kwenye mji mkuu.
Mara nyingi NATO imekuwa ikifanya mashambulizi wakati wa giza lakini hivi sasa kushambulia mchana ni jambo la kawaida. Shambulizi la ijumaa ni mwendelezo wa shambulizi lililoanza alhamisi usiku.
Wakati mashambulizi yakiwa yanaendelea kumekuwa na majaribio kadhaa ya kutaka kutatua mzozo uliodumu kwa miezi mitatu sasa huko Libya.
Mtoto wa Kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi amesema baba yake yuko tayari kufanya uchaguzi na kwamba atajiuzulu kama atashindwa. Waasi na Marekani wamekataa pendekezo hilo.
Wakati huo huo waziri mkuu wa Libya Baghdad al- Mahmoud,i amesema bwana Gadhafi hataachia madaraba kwa kuhofia shinikizo la kimataifa .