Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:07

David Cameron aahidi kusaidia kumsaka Gadhafi


Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron wakipeana mikono na wananchi wa Libya huko Benghazi, September 15, 2011.
Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron wakipeana mikono na wananchi wa Libya huko Benghazi, September 15, 2011.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameahidi kusaidia kumsaka Gadhafi

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameahidi kusaidia kumsaka kiongozi wa zamani wa Libya, Moammar Gadhafi na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

Bwana Cameron, Alhamis alitaka kiongozi huyo wa Libya aliyeondolewa madarakani na wafuasi wake wajisalimishe, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli. Kiongozi huyo wa Uingereza alizungumza akiwa pamoja na kiongozi mwenzake wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.

Rais wa Ufaransa amesema wakati alipowasili nchini Libya kwamba anamatumaini ya kupatikana demokrasia, amani na suluhisho katika nchi hiyo.Marais hao wawili ni wakuu wa kwanza wa nchi za kigeni kutembelea taifa hilo tangu kuangushwa kwa bwana Gadhafi. Walipokelewa kwa furaha nchini humo huku viongozi wote wakiwa maarufu miongoni mwa wa-Libya kwa kusaidia kumuondoa madarakani bwana Gadhafi.

XS
SM
MD
LG