Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 08:07

Wa-Liberia wapiga kura leo


Raia wa Liberia wakiwa kwenye harakati za kila siku za kutafuta riziki katika mji mkuu Monrovia, kabla ya upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa Jumanne

Raia wa Liberia wanapiga kura leo katika uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge kwa muhula wa pili baada ya kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe

Wa-Liberia wanajiandaa kwenda kwenye vituo vya kupigia kura kwa mara ya pili tangu kumalizika kwa miaka 14 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais Ellen Johnson Sirleaf anawania muhula wa pili katika upigaji kura Jumanne, siku chache baada ya kupokea tuzo ya amani ya Nobel.Licha ya kupewa heshima ya kimataifa, bibi. Sirleaf anakabiliwa na wakati mgumu katika uchaguzi huu.

Kiongozi huyo wa Liberia anashindana dhidi ya wapinzani zaidi ya darzeni moja, na mpinzani wake mkali anawania pamoja na mchezaji maarufu wa mpira wa miguu, George Weah.

Weah alikuwa wa pili katika uchaguzi wa mwaka 2005 na wakati huu anawania nafasi ya makamu Rais akiwa na Winston Tubman, ambaye sawa na bibi.Sirleaf, ni mhitimu kutoka chuo kikuu cha Harvard.

Upinzani unadai kwamba bibi Sirleaf ameshindwa kurekebisha madhara ya vita baada ya takribani miaka sita ya kuwepo madarakani. Wanazungumzia miundo mbinu iliyoharibiwa na vita na umaskini na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira.

Wapinzani pia wanamkosoa bibi. Sirleaf kwa rekodi yake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambapo yeye kwa wakati mmoja alimuunga mkono mbabe wa vita na Rais wa zamani Charles Taylor.

kama hakuna mgombea yeyote atakayeshinda wingi wa kura, duru ya pili itabidi kufanyika. Wa-Liberia pia watapiga kura kuchagua wabunge.

Wakosoaji wanahoji muda wa kutangazwa kwa tuzo ya Nobel hapo Ijumaa, ambapo bibi. Sirleaf alishinda pamoja na wanawake wawili wengine. Wanasema huwenda ikatoa matokeo yasiyo sawa.


XS
SM
MD
LG