Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:23

Liberia yaadhimisha miaka 169 ya Uhuru


Liberian President Ellen Johnson-Sirleaf
Liberian President Ellen Johnson-Sirleaf

Liberia siku ya Jumanne iliadhimisha miaka 169 tangu kupata uhuru wake. Hata hivyo, baadhi ya wananchi walisema hawakuona chochote cha kusherehekea kwa sababu ya hali ngumu ya maisha inayoletwa na kudorora kwa uchumi wa nchi hiyo.

Lakini balozi wa Liberia nchini Marekani, Jeremiah Sulunteh, alisema kuwa ingawa kuna changamoto, nchi hiyo imepiga hatua kubwa chini ya uongozi wa rais Ellen Johnson Sirleaf.

Balozi huyo alisema kuwa Waliberia wanasherehekea uhuru kwa kauli mbiu ya “kuunganisha maendeleo kwa lengo la kufanya mabadiliko ya Liberia.” Aliongeza kuwa jgenda ya kitaifa inayolenga kukamilika mnamo mwaka wa 2030, na inayoungwa mkono na rais Sirleaf, ni mpango wa muda mrefu na kwamba hatua zozote ambazo zitaleta mabadikliko nchini Liberia ni sharti zisherehekewe.

Sulunteh alisema kuwa serikali imepiga hatua kubwa kukarabati baadhi ya miundo mbinu nchini Liberia, iliyoharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

XS
SM
MD
LG