Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 28, 2023 Local time: 08:52

Leo ni uhuru wa Marekani


Fataki hupigwa saa za usiku katika sherehe za siku ya uhuru wa Marekani.

Marekani siku ya Jumatatu ya Julai nne inasheherekea miaka 240 ya uhuru wake kutoka kwa muingereza kwa sherehe mbali mbali za kitaifa ikijumuisha gwaride na kurushwa fataki nchi nzima.

Rais Barack Obama ni mwenyeji wa familia za wanajeshi kwenye nyama choma huko White House ikiambatana na tamasha litakalotumbuizwa na wanamuziki Kendrick Lamar na Janelle Monae. Kama mvua haitanyesha Jumatatu usiku mjini Washington kama ilivyotabiriwa wakazi watakuwa na mandhari nzuri ya kutazama fataki za mji mkuu zitakazoonyeshwa karibu na bustani ya kitaifa maarufu kama National Mall.

Lakini umuhimu wa sherehe hizi unaonekana kwenye mtaa kutoka White House hadi jengo la National Archives. Mahala ambapo ni makazi ya rasimu yalipotangaziwa uhuru na Thomas Jefferson.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG