Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:31

Waislamu duniani washerehekea sikukuu ya Eid Al- Haji


Baadhi ya waumini wa kiislamu katika sherehe za Eid Al Haji
Baadhi ya waumini wa kiislamu katika sherehe za Eid Al Haji

Waislamu duniani kote wanaendelea kuadhimisha sikukuu ya Eid Al-Haji au sherehe ya kutoa kafara, inayoadhimishwa mwishoni mwa Hija ambayo ni ibada ya kila mwaka inayofanyika mjini Mecca.

Mwaka huu, sikukuu hiyo inaadhimishwa Jumatatu huku baadhi ya nchi zikishsrehekea siku ya Jumanne.

Eid Al Haji ni sikukuu ya kuadhimisha uwamuzi wa mtume Ibrahim kukubali kutekeleza amri ya kumtoa mwanawe Ismael kafara kwa Mungu, na hapo Mungu kumpatia kondoo mchanga kama kafara mbadala.

Waislamu hutoa heshima kwa ukarimu wa Mungu kwa kuchinja mifugo na kutayarisha nyama yake ambayo huliwa wakati wa sikukuu hiyo.

Leo ni siku ya mapumziko katika nchi za Afrika Mashariki na kati ambako waislamu wanatembeleana na kusherehkea sikukuu hii moja wapo muhimu kwa waislamu.

XS
SM
MD
LG