Benki nchini humo, zinazokumbwa na mzozo wa kiuchumi kwa zaidi ya miaka miwili, zilifunguliwa kwa muda wiki iliyopita chini ya ulinzi mkali baada ya kufungwa kwa wiki nzima kufuatia uporaji mwingi wa wateja waliokata tamaa ya kupata pesa zao.
Ali Deeb al Sahili alilishikilia mateka tawi la benki moja katika mji wa Chatura ulio umbali wa kilomita 45 mashariki mwa mji mkuu Beirut, kulingana na shirika linalotetea wateja wa benki, akitaka kutuma pesa kwa mwanawe nchini Ukraine.
Mwanajeshi huyo aliyestaafu ambaye alikuwa na silaha, mwenye umri wa miaka 50, aliomba kupewa dola 24,000 zinazohifadhiwa kwenye akaunti yake.
Kaka yake amesema aliwekwa kizuizini, na haikufamika wazi ikiwa alifanikiwa kupata pesa yoyote ya akiba yake.