Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 04:51

Lavrov alaumu mataifa ya magharibi kwa hali ngumu ya kiuchumi ulimwenguni


Waziri wa mambo ya kigeni wa Russia Sergei Lavrov akiwa na mwenzake wa Ethiopia Demeke Mekonnen mjini Addis Ababa

Waziri wa mambo ya nje  wa Russia Sergei Lavrov Jumatano amekamilisha ziara yake barani Afrika akimalizia nchini  Ethiopia, huku akiyalaumu mataifa ya magharibi kutokana na hali ngumu ya uchumi inayoendelea kushuhudiwa kote ulimwenguni.

Wakati akiwa mjini Addis Ababa, Lavrov alikutana na naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia, Demeke Mekonnen, kwa mazungumzo kuhusu masuala kadhaa kama vile biashara na ushirikiano wa kijeshi, pia alikutana na wanadiplomasia mjini humo.

Wakati akiongea kwenye ubalozi wa Russia mjini Addis Ababa, Lavrov alisema kwamba bei za vyakula na mbolea zilipanda zaidi baada ya ulimwengu kukumbwa na janga la covid 19, na pia kwa sababu ya uwezo wa mataifa katika kufanya manunuzi ya ziada kufatia kuingia kwa janga.

Vile vile alilaumu sera za mataifa ya magharibi akizielezea kuwa mbovu. Aliongeza kwamba sera hizo mbovu zimesababisha kupanda kwa bei ya mbolea na hivyo kusababisha bei ya vyakula kupanda, huku akisema kwamba nchi yake inalengwa na magharibi akihofia kwamba China huenda ikafuata.

Alisema kwamba Uturuki pamoja na Umoja wa mataifa wanashauriana kuhusu kuumaliza mzozo wa chakula unaoyakumba mataifa mengi ya Afrika, kufuatia kile alichokitaja ni kutokana na Russia kuwekewa vikwazo.

Naibu waziri mkuu wa Ethiopia ambaye pia ni waziri wa mambo ya kigeni wa taifa hilo nje Demeke Mekonnen alisema kwamba wanakaribisha ushirikiano na Russia.

Wakati huo huo Lavrov alikutana na rais wa Ethiopia Sahlework Zewdie wakati akifanya mazungumzo naye kwa mujibu wa taarifa kutoka wizara ya mambo ya kigeni nje . Saa za jioni waziri wa Russia aliondoka Addis Ababa kuelekea nyumbani akikamilisha ziara ya mataifa manne barani Afrika.

XS
SM
MD
LG