Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 11, 2025 Local time: 04:48

Kuvuja nyaraka za siri kwaweza kuathiri mustakbali wa Marekani na washirika wake


FILE - Wizara ya Ulinzi ya Marekani iliyoko katika jengo la Pentagon huko Arlington, Virginia, nje ya jiji la Washington, April 19, 2019.
FILE - Wizara ya Ulinzi ya Marekani iliyoko katika jengo la Pentagon huko Arlington, Virginia, nje ya jiji la Washington, April 19, 2019.

Kuvuja hivi karibuni kwa darzeni ya nyaraka kadhaa za siri ya juu, ikiwemo tathmini za vita vya Ukraine iliyofanywa na Wizara ya Ulinzi, imeibua wasiwasi kuhusu taarifa zilizomo katika nyaraka hizo.

Nyaraka hizo zinaweza kuisaidia Russia katika vita vyake ilivyoanzisha mwaka 2022, na kwamba inaweza kuwa vigumu zaidi mashirika ya upelelezi ya Marekani kufanya kazi zake siku za usoni.

Miongoni mwa mambo mengine, nyaraka hizo ni pamoja na tathmini ya kina ya uwezo wa Ukraine na Russia na udhaifu wao katika uwanja wa mapambano, muda wa matarajio ya kufikisha mifumo mipya ya silaha, na kubainika kuwa ulinzi wa anga wa Ukraine unatia wasiwasi kutokana na upungufu wa silaha.

Taarifa hiyo iliyomo katika mafaili yaliyovujishwa inapendekeza kuwa huduma za kiupelelezi za Marekani zina taarifa za kina zisizo za kawaida za shughuli za jeshi la Russia, ikiipa Marekani uwezo wa kuyapa majeshi ya Ukraine taarifa za mapema za mashambulizi yanayosubiri kutekelezwa na wapi wajikite katika mashambulizi yao dhidi ya majeshi ya Russia.

Nyaraka hizo pia zinatoa mwanya kuonyesha ni kwa kiwango gani juhudi za Marekani katika kuisaidia Ukraine zilihusisha uratibu wa huduma mbalimbali za upelelezi za serikali ya Marekani na za kigeni, ambapo siyo wote wanakawaida kushirikiana kile walichogundua baina yao.

Kwa kuanza na ripoti iliyochapishwa na gazeti la The New York Times mwishoni mwa wiki iliyopita, waandishi wa habari na watafiti wamegundua darzeni ya nyaraka za siri nyingi kati ya hizo zinahusiana na vita vya Ukraine, zilizopachikwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ikwemo Discord – safu ya utumaji ujumbe maarufu kwa michezo ya kompyuta – Twitter na Telegram.

XS
SM
MD
LG