Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 09:59

Kutekwa nyara kwa madada watano wa Nigeria kumezua kilio cha kitaifa

Wasichana waliokuwa wametekwa nyara kutoka shule ya bweni iliyoko Kaskazini-Magharibi mwa jimbo la Zamfara huko Nigeria, wakipanda gari baada ya kuachiliwa Machi 2, 2021. Picha na REUTERS/Afolabi Sotunde

Kutekwa nyara kwa madada watano wa Nigeria karibu na Abuja kumezua kilio cha kitaifa na kuibua hofu kuhusu ukosefu wa usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Kutekwa nyara kwa madada watano wa Nigeria karibu na Abuja kumezua kilio cha kitaifa na kuibua hofu kuhusu ukosefu wa usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Madada hao walitekwa mwanzoni mwa mwaka na watu wenye silaha ambao waliivamia nyumba yao kilomita 25 kutoka katikati mwa jiji la Abuja, mwanafamilia mmoja aliiambia AFP.

Alisema washambuliaji walimuua dada mmoja, Nabeeha Al-Kadriyar mwenye umri wa miaka 21, wakati tarehe ya mwisho ya kutoa fedha zilizoombwa ilipopita. Mazungumzo yalikuwa yakiendelea ili wengine waachiliwe.

Utekaji nyara na kudai fidia limekuwa tatizo kubwa nchini Nigeria huku magenge ya wahalifu yakilenga barabara kuu, nyumba za makazi ya watu na hata kuwanyakua wanafunzi kutoka shule.

Forum

XS
SM
MD
LG