Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 05:01

Kutangazwa kwa mteule wa Trump na mvutano katika Seneti


Rais Donald Trump akihutubia mkutano kwenye uwanja wa Four Seasons huko Montana ExpoPark, Alhamisi, Julai 5, 2018.
Rais Donald Trump akihutubia mkutano kwenye uwanja wa Four Seasons huko Montana ExpoPark, Alhamisi, Julai 5, 2018.

Rais Donald Trump Jumatatu usiku atatangaza mteule wake kwenye Mahakama ya Juu ambaye atachukuwa nafasi ya Jaji anayestaafu Anthony Kennedy.

Tangazo hilo huenda likaanzisha mvutano mkubwa juu ya kumthibitisha mteule huyo katika Baraza la Seneti, ambapo Warepublikan wanawazidi wapinzani wao kwa idadi ndogo sana na Wademokrat wanasema wako tayari kwa mapambano juu ya uteuzi huo wa Trump katika kujaza nafasi hiyo.

Katika ujumbe wa Tweet Jumatatu, kabla ya kutangaza uteuzi huo, Trump alisema kuwa “muda mrefu amekuwa akisikia kuwa uamuzi muhimu zaidi ambao Rais wa Marekani anaweza kufanya ni kuteuwa Jaji wa Mahakama ya Juu.”

Katika hotuba yake kama rais ya kila wiki, Trump amesema kuwa “jukumu lake kubwa kabisa ni kumteuwa jaji ambaye atakuwa mkweli katika kutafsiri Katiba kama ilivyoandikwa.”

Rais ameahidi kumteuwa mtu ambaye anasifa stahili, uwezo mkubwa, hana maamuzi ya upendeleo na ni mwenye kuheshimu sheria na Katiba.”

Wakati wa mkutano wa kampeni huko Montana Alhamisi, Trump alikuwa anajaribu kuwapa matumaini wafuasi wake juu ya mteule wake.

“Kama mnavyojua hivi sasa kuna nafasi iliyokuwa wazi katika Mahakama ya Juu. Na kama mkinisikiliza Jumatatu nafikiri mtakuwa na furaha sana juu ya uteuzi huo.

Ni sawa? Na wote hao wako vizuri. Wote hao wako vizuri,” Trump aliueleza mkutano uliokuwa ukishangilia huko Great Falls, Montana.

XS
SM
MD
LG