Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:04

Kurudishwa tena uhusiano wa kidiplomasia kati ya Israel na Uturuki kutasaidia Wapalestina-Cavusoglu

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu akitembelea eneo la msikiti wa Al-Aqsa .(REUTERS).
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu akitembelea eneo la msikiti wa Al-Aqsa .(REUTERS).

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema, kurudishwa tena uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi yake na Israel kutasaidia Wapalestina,

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema, kurudishwa tena uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi yake na Israel kutasaidia Wapalestina, alisema hayo alipoanza ziara yake ya kwanza nchini Israel Jumatano akiwa mwanadiplomasia wa kwanza wa juu kutembelea Israel katika kipindi cha miaka 15.

Cavusoglu, ambaye alikutana na maafisa wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu siku ya Jumanne, alikuwa mjini Jerusalem wakati Uturuki na Israel zikijaribu kurekebisha uhusiano wao kufuatia mtafaruku ulioanza wakati wa operesheni ya kijeshi ya Israel huko Gaza mwaka 2008.

Cavusoglu na mwenzake wa Israel Yair Lapid walisisitiza kuwa uhusiano wa kiuchumi umeendelea kukua licha ya miaka mingi ya uhasama kati ya nchi hizo mbili.

"Hatutajifanya kuwa uhusiano wetu haujaona kupanda na kushuka," Lapid alisema.

"Hata wakati wa mvutano wa kisiasa, ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi zetu umekuwa ukiongezeka kila mara."

Cavusoglu alibainisha kuwa Uturuki ilikuwa mshirika 10 bora wa kibiashara wa Israel na kivutio kikuu cha watalii wa Israel, akitoa matumaini kuwa kuimarika kwa uhusiano kunaweza kuleta manufaa kwa Wapalestina.

XS
SM
MD
LG