Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:47

Kura zahesabiwa Senegal


mtu akipiga kura wakati wa uchaguzi wa urais katika mji mkuu Dakar, February 26, 2012 huko senegal.
mtu akipiga kura wakati wa uchaguzi wa urais katika mji mkuu Dakar, February 26, 2012 huko senegal.

Wapinzani wanataka rais aliyoko madarakani atoke.

Maafisa wa uchaguzi nchini Senegal wanahesabu kura za uchaguzi wa urais uliofanyika jumapili. Wagombea wa upinzani wanataka kumuondoa rais Abdoulaye Wade ambaye amewakasirisha wasenegali wengi baada ya kuongeza muda wake wa utawala wa miaka 12 katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Matokeo ya awali yasiyo rasmi yanaonesha ushindi wa karibu na afisa wa kampeni wa mmoja wa wapinzani wakubwa wa bwana Wade Macky Sall alisema jumatatu kuwa uchaguzi wa duru ya pili unaweza kufanyika. Uamuzi wa bwana Wade wa kugombea muhula wa tatu umesababisha maandamano ya wiki kadhaa sasa kabla ya upigaji kura . wapinzani wanasema uamuzi wake ni kinyume cha katiba kufuatia marekebisho ya sheria ya katiba mwaka 2001 ambayo yanamtaka rais kukaa madarakani kwa mihula miwili tu.

XS
SM
MD
LG