Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 02:39

Wamarekani wanaendelea na uchaguzi wa awali


Voters walk to a polling precinct on primary day in Florida for the U.S. presidential election in Boca Raton, Florida, March 15, 2016..

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa katika majimbo matano ya Marekani leo hii.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa katika majimbo matano ya Marekani leo hii ambapo wapiga kura watachagua wagombea urais katika kura za awali huku Mrepublikan, Donald Trump, na Mdemokrat, Hillary Clinton, wakitafuta kura zaidi za kuongoza wakati wapinzani wao wakijaribu kuleta uhai ili kuendelea na kampeni zao.

Jimbo la Florida ndilo muhimu katika kura za leo ambapo mshindi wa Republikan atapata wajumbe 99.

Uchunguzi wa maoni wa Jumatatu ulionyesha bwana Trump anaongoza kwa karibu asilimia 17 dhidi ya mpinzani wake ambaye ni Seneta wa Florida Marco Rubio ambaye anahitaji kushinda ili kuleta uhai katika harakazi zake za kugombea kiti cha kukiwakilisha chama cha Republikan katika uchaguzi wa Urais wa Marekani.

XS
SM
MD
LG