Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 28, 2023 Local time: 13:23

Kura ya urais bado inahesabiwa Sierra Leone


Maafisa wa uchaguzi wakihesabu kura ya kiti cha urais huko Sierra Leone

Zoezi la kuhesabu kura kwenye duru ya marudio ya uchaguzi wa urais huko Sierra Leone linaendelea. Wananchi walipiga kura Jumamosi na Rais aliyepo madarakani Ernest Bai Koroma anatarajiwa kuachia madaraka mwaka huu baada ya kuhudumu mihula yake miwili inayokuwa na kipindi cha miaka mitano kila mmoja.

Wananchi walipiga kura kuchagua baina ya mgombea wa chama tawala cha All People’s Congress, Samura Matthew Wilson Kamara na mgombea wa upinzani wa chama cha Sierrra Leone Peoples Party, Julius Maada Bio. Hii ni mara ya pili kwa mgombea wa upinzani Bio kuwania kiti cha urais. Alishindwa kwenye uchaguzi wa 2012 na Rais aliyepo madarakani hivi sasa Ernest Bai Koroma.

Ripoti zinaeleza idadi ya watu waliojitokeza ilikuwa ndogo ikilinganishwa na upigaji kura wa mara ya kwanza, huwenda kwa sababu ya tahadhari ya usalama. Ripoti za vyombo vya habari zinasema uendeshaji magari ulipigwa marufuku katika baadhi ya maeneo hali iliyolazimisha wapiga kura kutembea kwenda kwenye vituo vyao vya kupiga kura.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG