Jaji Peter Lane, amesema katika Mahakama Kuu kwamba uamuzi wa kuondoa ulinzi kwa Harry kwa msingi wa tukio kwa tukio haukuwa kinyume cha sheria, usio na maana au usio na haki.
Duke wa Sussex alidai kuwa yeye na familia yake walikuwa hatarini wakati alipoitembelea Uingereza, kwa sababu ya chuki dhidi yake na mkewe kwenye mitandao ya kijamii na kuwindwa bila kuchoka na vyombo vya habari.
Wakili wake amesema kwamba kikundi cha serikali ambacho kilikagua mahitaji ya usalama ya Harry, kilifanya vibaya na kushindwa kufuata sera zake ambazo zingehitaji uchambuzi wa hatari ya usalama wa mwana mfalme huyo.
Forum