Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:55

Kundi la Taliban linashirikiana na Al-Qaeda lakini linakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Islamic state


Wapiganaji wa Taliba
Wapiganaji wa Taliba

Ripoti ya wataalam wa umoja wa mataifa imesema kwamba viongozi wa Taliban nchini Afghanistan, wanaendelea kushirikiana kwa karibu sana na kundi la kigaidi la Al-Qaeda, wanapoendelea kudhibithi uongozi wao nchini humo.

Ripoti hiyo inasema kwamba tishio kubwa kwa utawala wa Taliban ni kundi la Islamic state na mamluki waliokuwa wanawashambulia maafisa wa usalama wa serikali ya Afghanistan iliyoondoka madarakani.

Ripoti hiyo ambayo imewasilishwa kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa, vile vile inaonya kwamba huenda mashambulizi yakaongezeka wakati wa hali nzuri ya hewa, kati ya wapiganaji wa kundi la Islamic state na Taliban.

Viongozi wa Taliban wameteua watu 41 katika baraza lake la mawaziri na nafasi nyingine serikalini, waliowekewa vikwazo na umoja wa mataifa

XS
SM
MD
LG