Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 13:37

Kundi la mamluki wa Russia, Wagner ladai kuuteka mji wa Ukraine wenye madini


Mkuu wa kundi la Wagner, mfanyabiashara Yevgeny Prigozhin
Mkuu wa kundi la Wagner, mfanyabiashara Yevgeny Prigozhin

Kiongozi wa kampuni binafsi ya kijeshi ya Russia wa kundi la Wagner Jumanne amesema wanajeshi wake waliuteka mji wa Ukraine wenye madini wa Soledar lakini mapigano yalikuwa yakiendelea, mashirika ya habari ya Russia yameripoti.

Mapema Jumanne, Ukraine ilisema wanajeshi wake walikuwa bado wanaushikilia mji huo licha ya uvamizi wa Russia.

“Vitengo vya Wagner vilichukua udhibiti wa eneo lote la Soledar. Kikosi kimepangwa katikati mwa mji huo ambako mapigano yanaendelea,” mkuu wa Wagner Yevgeny Prighozin alisema katika taarifa iliyonukuliwa na mashirika ya habari ya Russia.

Aliongeza kuwa “idadi ya wafungwa itatangazwa Jumatano”, bila ya kutoa maelezo zaidi.

XS
SM
MD
LG