Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 06:20

Kundi la mamluki wa Russia ladai kuuzingira mji wa Ukraine wa Bakhmut


Ofisi ya kundi la Wagner mjini Saint Petersburg
Ofisi ya kundi la Wagner mjini Saint Petersburg

Yevgeny Prigozhin, muanzilishi wa kundi la mamluki la Russia la Wagner, amesema katika video iliyochapishwa leo Ijumaa kwamba mji wa Ukraine wa Bakhmut umezingirwa na wapiganaji wake na kwamba wanajeshi wa Kyiv wanadhibiti barabara moja peke yake.

Mamluki wa Prighozin wamekuwa wakifanya mashambulizi mashariki mwa Ukraine kwa miezi kadhaa pamoja na wanajeshi wa Moscow kujaribu kuuteka mji wa Bakhmut, ikiwa kama hatua muhimu kujaribu kuteka pia miji mikubwa kama Kramatorsk na Sloviansk.

Prigozhin akiwa amevalia sare za kijeshi, katika ujumbe wa video ametoa wito kwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kuondoa wanajeshi wake katika mji huo mdogo.

Prighozin amesema wapiganaji wake wanapambana na wazee na watoto badala ya kukabiliana na jeshi la Ukraine.

XS
SM
MD
LG