Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 05:31

Kundi la kijeshi la Guinea kutangaza mikakati kuelekea utawala wa kiraia


Kanali Mamady Doumbouya akitoa hotuba kwenye mji mkuu wa Guinea wa Conakry
Kanali Mamady Doumbouya akitoa hotuba kwenye mji mkuu wa Guinea wa Conakry

Kundi la kijeshi lililofanya mapinduzi kwenye taifa la Afrika magharibi la Guinea Jumanne limetoa wakaraka unaoahidi kurejesha taifa hilo kwenye utawala wa kiraia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, waraka huo ambao ulisomwa kwenye televisheni ya kitaifa mida ya jioni imeelezea masuala kadhaa kama kuandikwa kwa rasimu ya katiba mpya, kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki, ingawa haijaeleza muda ambao hayo yanatarajiwa kufanyika.

Waraka huo pia umeelezea kuhusu taasisi nne za kiserikali ambazo zitaongoza serikali ya mpito. Ya kwanza ni kamati ya kitaifa ya maendeleo au CNRD itakayoongozwa na kiongozi wa mapinduzi Mamady Doumbouya akiwa kama rais wa mpito pamoja na mkuu wa majeshi, serikali itakayoongozwa na waziri mkuu pamoja na bunge la mpito likijulikana kama National Transition Council au CTN.

Kundi la wanajesji likiongozwa na Doumbouya septemba 5 lilimuondoa madarakani rais Alpha Conde mwenye umri wa miaka 83, ambaye katika miezi ya karibuni alikuwa akikabiliwa na kushuka kwa umaarufu wake kutokana na hali ngumu ya maisha nchini humo.

XS
SM
MD
LG