Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:14

Islamic State yapoteza himaya


Vikosi vya usalama vya Iraqi vikishikilia bendera ya Islamic State baada ya kuishusha chini katika jimbo la Anbar.
Vikosi vya usalama vya Iraqi vikishikilia bendera ya Islamic State baada ya kuishusha chini katika jimbo la Anbar.

Kundi la wapiganaji wa Islamic State limepoteza asilimia 22 ya eneo lake katika miezi 15 iliyopita huku asilimia 8 ikiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Ongezeko la shinikizo la kijeshi dhidi ya kundi la wapiganaji wa Islamic State kote Syria na Iraq kumepelekea kundi hilo kupoteza asilimia 22 ya eneo lake katika miezi 15 iliyopita huku asilimia 8 ikiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Hayo ni matokeo ya uchunguzi uliofanywa na shirika la HIS ambalo limesema kundi hilo linaendelea kutengwa na kukataliwa.

HIS imeeleza eneo la kaskazini mwa Syria kati ya makao makuu waliyojitangazia Islamic State ya Raqqa na mpaka wa Uturuki ambapo mashambulizi ya anga kutoka Russia na muungano unaoongozwa na Marekani wakiungana na wapiganaji wa Kisunni na Kikurdi ili kuwasukuma wanamgambo na kufungua mipaka muhimu. Kundi la Islamic State kwa sasa linashikilia eneo dogo la Syria ambapo wanaweza kuingiza vifaa na wapiganaji kutoka Uturuki.

XS
SM
MD
LG