Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 12:03

Kudhibitiwa kwa bandari za Ukraine kumesababisha bei za bidhaa kupanda duniani kote - FAO


Mwanajeshi anayeshirikiana na vikosi vya Russia katika eneo la Donetsk, Ukraine.
Mwanajeshi anayeshirikiana na vikosi vya Russia katika eneo la Donetsk, Ukraine.

Shirika la chakula na kilimo ulimwenguni FAO limesema bei ya chakula duniani imebadilika na kuwa nzuri mwezi uliopita kwa kiwango cha juu sana lakini ilikuwa chini kidogo mwezi machi ambapo kulishuhudiwa kupanda kwa bei ya juu zaidi ya vyakula kuwahi kutokea.

Maafisa wa FAO wanaona matumaini madogo ya kupungua kwa bei ya chakula mradi tu kama vita vya Russia na Ukraine vitaendelea.

Nchi zote mbili kwa pamoja zinachangia karibu theluthi moja ya mauzo ya ngano nje ya nchi na aina nyingine za nafaka na hadi asilimia 80 ya usafirishaji wa mafuta ya alizeti.

Naibu mkurugenzi wa FAO katika kitengo cha masoko na biashara, Joseph Schmi-dhuber, anasema kuvurugika kwa mauzi ya bidhaa hizo na nyingine za chakula kutoka Ukraine kunaathiri sana usalama wa chakula duniani.

Anasema nchi masikini zinataabika zaidi kwa sababu zinauza nje ya soko. Nchini Ukraine kuna zaidi ya tani milioni 25 za nafaka ambazo haziwezi kusafirishwa nje kwa sababu ya ukosefu wa miundombinu na vizuizi kwenye bandari.

Hata hivyo pamoja na hali ya vita inayoendelea nchini humo mazao ya nafaka kama vile mahindi, na ngano yatavunwa mwezi Julai na Ugusti. Anasema takriban tani milioni 14 za nafaka zinaweza kuwa tayari kwa usafrishaji nje.

Afisa huyo wa FAO anasema hali nchini Ukraine inaonesha kwamba tatizo la sasa sio ukosefu wa chakula lakini ni jinsi ya kukifikia. Anasema kuna nafaka za kutosha kulisha dunia, isipokuwa tatizo ni chakula hakiwezi kwenda kwenye maeneo yanayohitajika.

XS
SM
MD
LG