Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 09:58

11 kuchunguza jaribio la mapinduzi la Gambia


Rais wa Gambia, Adama Barrw katikati akikwagua gwaride mapema mwaka 2022.
Rais wa Gambia, Adama Barrw katikati akikwagua gwaride mapema mwaka 2022.

Gambia Jumanne iliunda jopo la uchunguzi na kuipa siku 30 kuripoti kuhusu jaribio la mapinduzi la wiki jana kufuatia kukamatwa kwa wanajeshi zaidi.

Jumatano iliyopita serikali ilisema ilizuia jaribio la mapinduzi na baadaye kuwaweka kizuizini baadhi ya wanajeshi.

Kapteni na Luteni wa jeshi walikamatwa mwishoni mwa juma na kusaidia wachunguzi kuibua madai ya mipango ya kuipindua serikali ya Rais Adama Barrow, msemaji wa serikali Ebrima Sankareh alisema katika taarifa yake ya Jumatatu.

Wanajeshi wengine watano wameshikiliwa, huku wengine wawili wanaotuhumiwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi bado wanasakwa.

Mwanasiasa wa upinzani Momodou Sabally, waziri wa zamani wa masuala ya rais chini ya kiongozi wa zamani Yahya Jammeh, pia yuko kizuizini baada ya kuonekana kwenye video inayopendekeza rais wa sasa angepinduliwa kabla ya uchaguzi ujao wa serekali za mitaa.

Chama cha Sabally cha United Democratic Party kimetoa wito wa kuachiliwa kwake mara moja.

Jopo la wapelelezi la watu 11, wakiwemo maafisa wa wizara ya sheria, ofisi ya usalama wa taifa, vikosi vya jeshi, polisi na idara za ujasusi, waliapishwa Jumanne kwa ajili ya uchunguzi huo.

Jopo hilo lina siku 30 kuanzia Jumanne kuchunguza, kuandaa na kuwasilisha ripoti yao ya njama ya mapinduzi.

Afrika Magharibi imetikiswa na mfululizo wa mapinduzi ya kijeshi tangu mwaka 2020, nchini za Mali, Guinea na Burkina Faso zipo chini ya serekali za kimapinduzi.

XS
SM
MD
LG