Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 18:27

Sessions aapishwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani


Rais Donald Trump akiangalia Makamu wa Rais Mike Pence (kushoto) akimwapisha Mwanasheria Mkuu Jeff Sessions (Kulia), ofisi ya Oval, White House, Washington.
Rais Donald Trump akiangalia Makamu wa Rais Mike Pence (kushoto) akimwapisha Mwanasheria Mkuu Jeff Sessions (Kulia), ofisi ya Oval, White House, Washington.

Baraza la Seneti la Marekani lilimpitisha Sessions Jumatano, baada ya majadiliano ya zaidi ya siku moja na malumbano makali yaliyopelekea kuzuiwa kwa mdemokrat maarufu kushiriki katika majadiliano hayo.

Kura 52 dhidi ya 47 zilimwezesha Sessions, Seneta wa Repablikan wa muda mrefu anayewakilisha jimbo la Alabama, kuwa mwanasheria wa ngazi ya juu na mteule wa baraza la mawaziri wa sita aliyepitishwa katika uongozi mpya wa Rais Donald Trump.

“Hii ni “heshima ya kipekee,” Sessions aliwaambia maseneta wenzake katika hafla ya kumuaga baada ya kupitishwa. “Ni matarajio yangu na ombi langu kwamba nitaendelea kuwa mwenye kuweza kutekeleza dhamana mliyonipa. Nitafanya kila nitakaloweza kutekeleza dhamana hiyo.”

“Sisi sote tunamfahamu yeye kuwa mtu mwenye maadili ya hali ya juu, mtu anayeheshimu neno lake, na mtu ambaye dhamira yake ni kutenda haki, uadilifu na kufuata sheria,” amesema mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti, Mrepablikan Chuck Grassley wa Iowa.

XS
SM
MD
LG