Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Agosti 19, 2022 Local time: 15:15

Kremlin yasema iko wazi kujadili suala la nyota wa mpira wa kikapu Griner


Brittney Griner akifikishwa mahakamani.

Kremlin imesema Ijumaa kuwa iko wazi kufanya mazungumzo juu ya uwezekano kwa kubadilishana wafungwa suala linalomhusisha nyota wa mpira wa kikapu Brittney Griner lakini iliionya Washington dhidi ya kutangaza suala hilo.

Griner, mshindi wa Marekani wa Olimpiki kwa mara mbili na nyota kwa mara nane wa Phoenix Mercury katika WNBA , alishikiliwa nchini Russia tangu Februari 17 baada ya polisi katika uwanja wa ndege wa Moscow kusema wamemkuta na kichupa chenye mafuta ya bangi katika mkoba wake.

Jaji alimhukumu mwanamichezo huyo mwenye umri wa miaka 31 Alhamisi kwa kumiliki na kuingiza kwa magendo dawa za kulevya na hivyo a kumpa adhabu ya kifungo cha miaka tisa jela. Kesi yenye ushawishi wa kisiasa imetokea wakati kuna mivutano kati ya Moscow na Washington kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Alipoulizwa huko White House Ijumaa kuhusu uwezekano wa kufikia muafaka wa kuachiliwa Griner, Rais Joe Biden alisema: “Nina matumaini… Tunafanya jitihada kubwa.”

Katika hatua isiyo ya kawaida, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alizungumza wiki iliyopita na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov, akimsihi akubali kufikia makubaliano ambapo Griner na Paul Whelan, Mmarekani aliyefungwa Russia kwa tuhuma za ujasusi, waachiliwe huru.

Lavrov na Blinken wote walikuwa nchini Cambodia Ijumaa kwa mkutano wa Jumuiya ya Mataifa ya Asia Kusini Mashariki. Blinken hakumuangalia mwenzake wakati wakikaa katika mkutano huo wa viongozi wa Asia Mashariki.

Lavrov aliwaambia waandishi wa habari kuwa Blinken hakujaribu hata kuwasiliana naye wakati walipokuwa wanahudhuria mkutano wa ASEAN.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG