Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:54

Kremlin inasema 'hakuna mikataba yoyote'iliyosainiwa kati ya Putin na Kim


Rais wa Russia Vladimir Putin akutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un katika mkoa wa kusini wa Amur, nchini Russia, Septemba 13, 2023.

Kremlin leo Ijumaa imesema hakuna mikataba iliyosainiwa wakati wa ziara inayoendelea nchini Russia ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari “ Hakuna mikataba iliyosainiwa wala hakuna mpango wa kusaini mkataba wowote.”

Awali, Marekani ilielezea wasiwasi wake kwamba nchi hizo mbili huenda zimeandaa makubaliano ya mauzo ya silaha.

Kim alianza ziara yake nchini Russia siku ya Jumanne.

Katika mkutano na Rais Vladimir Putin siku ya Jumatano, viongozi hao wawili walibadilishana zawadi za bunduki, jambo ambalo linaonekana kama ishara kufuatia wasiwasi wa nchi za Magharibi.

Putin alizungumzia matarajio ya ushirikiano mkubwa na Korea Kaskazini na kusema kuna “uwezekano” wa ushirikiano wa kijeshi licha ya vikwazo vya kimataifa dhidi ya Pyongyang.

Kremlin Alhamisi ilisema Putin alikubali mwaliko wa Kim kuitembelea Korea Kaskazini, bila ya kutangaza lini ziara hiyo itafanyika.

Leo, Kim alitembelea kiwanda kinachotengeneza ndege za kivita huko mashariki ya mbali nchini Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG