Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 00:02

Korea Kaskazini yaweka marufuku ya kuingia kwa wasafiri kutoka China kutokana na maambukizi ya Covid 19


Wasafiri waliovaa barakoa wapiga foleni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing, Disemba 29, 2022. Picha ya AP
Wasafiri waliovaa barakoa wapiga foleni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing, Disemba 29, 2022. Picha ya AP

Kufuatia ongezeko la hofu ya kimataifa juu ya wimbi la maambukizi ya Covid 19 linaloikumba China, Korea Kaskazini imeweka marufuku kwa wasafiri kutoka mshirika wake wa karibu na jirani.

“Raia wa China wamepigwa marufuku ya muda kuingia,” inasomeka taarifa kwenye tovuti ya idara ya kitaifa ya uhamiaji.

“Wale waliowasili hivi karibuni kutoka Jamhuri ya watu wa China, wakiwemo raia wa Korea Kaskazini, lazima wapitie karantini ya siku 30 kwa ajili ya uchunguzi.”

Haijabainika ni lini Korea Kaskazini iliweka marufuku hiyo au itaendelea kutelekelezwa kwa muda gani.

Nchi kadhaa zilitangaza masharti mapya kwa wasafiri kutoka China tangu Beijing kutangaza wiki hii kumalizika kwa karantini ya lazima kwa wasafiri wa ndani ya nchi na kuruhusu baadhi ya Wachina kusafiri nje ya nchi, na kusababisha hamu kubwa ya kusafiri nje ya nchi kwa wingi kwa Wachina.

XS
SM
MD
LG