Maafisa wa Marekani wanasema Korea Kaskazini imewaachia huru Wamarekani Kenneth Bae na Matthew Todd Miller na kwamba wawili hao wako njiani kurudi nyumbani.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Jen Psaki alitoa taarifa hiyo Jumamosi akikaribisha kuachiwa kwao.
Alisema mkurugenzi wa idara ya kitaifa ya ujasusi James Clapper alijadilia swala la kuachiwa kwa Wamarekani hao wawili na maafisa wa Korea Kaskazini. Marekani kwa muda mrefu imetoa mwito kwa Korea Kaskazini kuwaachia huru Wamarekani hao kwa misingi ya kibinadamu.
Tangazo la kuwaachia huru Bw. Bae na Bw. Miller limetolewa wiki chache baada ya hatua isiyotegemewa ya kumwachia huru M’marekani mwingine Jeffrey Fowle aliyekuwa kizuizini huko Korea Kaskazini.