Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 08:46

Korea kaskazini yatuma ndege ya kivita karibu na Korea kusini


Picha ya maktaba ya ndege ya kijeshi.
Picha ya maktaba ya ndege ya kijeshi.

Jeshi la Korea kusini limesema kuwa limetuma ndege zake za kivita Ijumaa baada ya kugundua ndege ya kijeshi aina ya 180 ya Korea kaskazini ilikuwa imetumwa kwenye mpaka wa kaskazini.

Hilo limefanyika wakati hali ya taharuki ikendelea kuongezeka kwenye Peninsula ya Korea. Ripoti zimeongeza kuwa ndege hiyo ya Korea kaskazini ilionekana kwenye sehemu tofauti karibu na ufukwe wa mataifa yote mawili kwa takriban saa nne, kulingana na mkuu wa jeshi la Korea kusini.

Ameongeza kuwa Korea kaskazini ilituma ndege 80 za kivita ikiwemo ile isiyoonekana kwa urahisi ya F-35A. Mwezi uliyopita, Korea kaskazini ilituma takriban ndege 10 za kivita karibu na mpaka wa kusini, hatua iliyopelekea operesheni ya kujilinda ya kijeshi kutoka Korea kusini.

Kando na ndege za kivita zilizotumwa mapema leo na Korea kusini, kuna nyingine takriban 240 za Marekani pamoja na taifa hilo zinazoendelea na mazoezi ya pamoja kwenye eneo hilo. Tangu Jumatano, Korea kaskazini imerusha makombora 30 baadhi yakipelekea kulia kwa ving’ora vya dharura nchini Korea kusini na Japan.

XS
SM
MD
LG