Korea Kaskazini, imetoa heshima kwa kiongozi wake wa zamani Kim Jong II katika siku yake ya kuzaliwa Jumatatu.
Kiongozi huya kama angekuwa hai angetimiza umri wa miaka 73.
Heshima hizo zilitolewa kwa kusheherekea mafanikio yake ya kisiasa na upinzani wake dhidi ya Marekani.
Nje ya Korea Kaskazini, makundi ya haki za binadamu yanataka ulimwengu ukumbuke yale yaliyofanywa na kiongozi huyo dikteta.
Makundi hayo yameainisha kama uvunjwaji wa haki za binadamu, kufanyisha watu kazi kwa nguvu, na kusababisha baa la njaa kwa umma.
Heshima kwa marehemu Kim Jong II, zilianza kwa milipuko mingi ya fataki mjini Pyongyang.