Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 12:32

Korea Kaskazini yathibitisha kifo cha kwanza cha Covid 19, shughuli zote zafungwa kudhibiti maambukizi


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akionekana amevaa barakoa kwa mara ya kwanza wakati wa mkutano na maafisa wa serikali mjini Pyongyang, May 12, 2022. Picha ya AP

Shirika la habari la Korea Kaskazini (KCNA) leo Ijumaa limethibitisha kifo cha kwanza cha Covid 19, ikiwa takwimu za kwanza kutolewa rasmi siku moja baada ya nchi hiyo kuthibitisha mlipuko wa kwanza wa Covid tangu janga hilo lianze.

Watu 187,800 hivi sasa wanapatiwa matibabu wakiwa wametengwa baada ya homa isiyojulikana kusambaa nchini kote tangu mwezi Aprili, KCNA imeripoti.

Watu 350,000 walionyesha dalili za homa hiyo, 162,200 kati yao walitibiwa. Lakini KCNA haikufafanua ni wangapi waligundulika na maambukizi ya Covid 19.

Sita walioonyesha dalili za homa hiyo walifariki, ilithibitishwa kwamba mmoja kati yao aliambukizwa aina ya kirusi cha Omicron, KCNA imesema.

Hayo ni wakati kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UN Alhamisi aliamuru kufungwa kwa shughuli zote kote nchini kama njia ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona yanayosababishwa na kirusi cha Omicron ambacho kinaambukiza kwa kasi.

Kugunduliwa kwa kirusi cha omicron kunatokea wakati Korea Kaskazini ndiyo nchi pekee duniani ambayo haijaanzisha zoezi la kuchanja raia wake milioni 26.

Kim Jong UN ameonekana kwa mara ya kwanza akiwa amevaa barakoa kwenye mkutano na maafisa wa serikali mapema Alhamisi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG