Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 23:43

Korea Kaskazini yarusha makombora ya masafa marefu


Mtu atazama silaha ya Korea Kaskazini kwenye televisheni mjini Seoul, Kore Kusini. Nov. 17,2022
Mtu atazama silaha ya Korea Kaskazini kwenye televisheni mjini Seoul, Kore Kusini. Nov. 17,2022

Ikiwa ni  majibu ya ongezeko la shughuli za kijeshi kutoka Marekani na washirika wake, Korea Kaskazini Ijumaa imerusha kombora la  masafa marefu na kupelekea kambi ya  jeshi la anga  la Japan na Marekani kutoa ilani ya tahadhari.

Kombora hilo maarufu kama Intercontinental Ballistic Missile- ICBM limeruka kwa zaidi ya muda wa saa moja na kisha kuangukia kwenye eneo la kiuchumi la Japan, takriban kilomita 200 magharibi mwa Hokkaido, kaskazini mwa taifa hilo, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa Japan.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, kituo cha kijeshi cha wanahewa cha Misawa kinachomilikiwa na Marekani na Japan katika kisiwa cha kaskazini cha Honshu kimesema kwamba ilani ya kuchukua tahadhari imetolewa kama hatua ya kujilinda bila kuitaja silaha iliyorushwa na Korea Kaskazini.

Hapa mjini Washington, baraza la kitaifa la usalama limesema kwamba jaribio hilo ni kinyume na mapendekezo ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kwamba linaongeza hali ya taharuki katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG