Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:14

Korea Kaskazini yarusha makombora ya balistiki kupinga kuwasili kwa nyambizi za Marekani Korea Kusini


Picha ya kombora la Korea Kaskazini iliyorusha ikionyeshwa katika kipindi cha habari katika televisheni kwenye kituo cha treni mjini Seoul, Korea Kusini Julai 25, 2023.

Korea Kaskazini imerusha makombora ya balistiki mawili ya masafa mafupi upande wa mashariki wa bahari yake, jeshi la Korea Kusini lilisema Jumanne.

Tukio hili limeongeza mwenendo wa hivi karibuni wa majaribio ya silaha ambapo kwa hakika ni kupinga kuwasili kwa vifaa vya jeshi la majini vikubwa vya Marekani huko Korea Kusini, likionyesha uwezo wake.

Katika duru ya tatu ya kurusha makombora tangu wiki iliyopita, Korea Kaskazini ilirusha makombora kabla ya saa sita usiku kutoka eneo karibu na mji mkuu wake, Pyongyang, Wakuu wa Wafanyakazi wa Jeshi wa Korea walisema. Ilisema makombora yote yalisafiri umbali wa karibu kilomita 400 kabla ya kutua katika maji nje ya pwani ya mashariki ya Rasi ya Korea.

Taarifa yake iliyaita makombora yaliyorushwa na Korea Kaskazini kuwa ni “uchokozi wa hali ya juu” unaotishia amani ya eneo na utulivu wake.

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida alisema serikali yake imetuma pingamizi kwa Korea Kaskazini juu ya makombora hayo yaliyorushwa, ambapo kwa kawaida hupitia ubalozi wake mjini Beijing.

Alisema Toky0 ilikuwa inafanya kila iwezalo kuchukua tahadhari wakati ikianzisha ushirikiano wa kiusalama wa pande tatu pamoja na Washington na Seoul.

Hakuna uharibifu ulioripotiwa kuhusiana na makombora hayo, ambayo, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Japan, yalianguka nje ya eneo maalum la kiuchumi la nchi hiyo.

Urushaji makombora hayo umefanyika saa kadhaa baada ya jeshi la majini la Korea Kusini kusema kuwa nyambizi ya Marekani inayoendeshwa kwa nguvu ya nyuklia iliwasili katika bandari ya Kisiwa cha Jeju.

Hilo liliainisha juhudi za wakishirika kuongeza muonekano wa vifaa vya kimkakati vya Marekani katika eneo ili kuitishia Korea Kaskazini.

Wiki iliyopita USS Kentucky ilikuwa ni nyambizi ya kwanza ya Marekani yenye silaha za nyuklia kuwasili Korea Kusini tangu miaka ya 1980.

Nyambizi ya Marekani yenye kubeba makombora ya balistiki USS Kentucky ikitia nanga huko katika kituo cha jeshi la majini cha Busan, Korea Kusini Julai 19, 2023. WOOHAE CHO/Pool via REUTERS
Nyambizi ya Marekani yenye kubeba makombora ya balistiki USS Kentucky ikitia nanga huko katika kituo cha jeshi la majini cha Busan, Korea Kusini Julai 19, 2023. WOOHAE CHO/Pool via REUTERS

Korea Kaskazini imejibu kuwasili kwake kwa kufanya majaribio ya makombora ya balistiki na ya masafa marefu wiki iliyopita ikiwa ni kuonyesha kwa namna fulani kuwa inaweza kufanya mashambulizi ya nyuklia dhidi ya Korea Kusini na meli za kijeshi za Marekani.

Korea kaskazini wiki hii itamkaribisha waziri wa ulinzi wa Russia na ujumbe wa ngazi ya juu wa China mjini Pyongyang kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya vita vya

Korea, vyombo vya habari vya serikali vimesema Jumanne ikionyesha ishara kwamba inaweza kufungua tena mipaka yake kwa wageni wa ngazi ya juu baada ya kufungwa kwa muda mrefu kutokana na janga la virusi vya corona.

Ujumbe wa kijeshi wa Shirikisho la Russia ukiongozwa na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu, utafanya ziara ya pongezi kwa DPRK, Shirika la Habari la Korea lilisema siku moja baada ya kuthibitisha ujumbe wa China, pia utahudhuria hafla hiyo ya Alhamisi.

Russia moja ya washirika wa kihistoria wa Pyongyang anaendelea kuwa moja ya mataifa machache ambayo yanadumisha uhusiano wa kirafiki na Korea Kaskazini na kiongozi wake Kim Jong Un, ambaye hivi karibuni ameelezea uungaji mkono wake Moscow kuivamia Ukraine, ikiijumuisha Washington, anasema sambaza roketi na makombora.

China, mshirika mkuu wa kibiashara wa Korea Kaskazini pia imethibitisha leo Jumanne kwamba itapeleka ujumbe unao-ongozwa na mwanachama wa Politburo, Li Hongzhong.

Wageni hao wa nchi za nje wanatarajiwa kuhudhuria hafla mjini Pyongyang kuadhimisha miaka 70 tangu kutiwa saini kwa mkataba wa kusitisha mapigano unaojulikana kama Victory Day huko Kaskazini ambapo KCNA inasema itaadhimishwa kwa matukio mazuri ambayo yatawekwa katika historia.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG