Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 19:58

Korea Kaskazini yafanya majaribio ya makombora


Televisheni zikionyesha picha za maktaba za majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini kwenye kituo cha treni mjini Seoul, Korea Kusini, Septemba 28, 2022.
Televisheni zikionyesha picha za maktaba za majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini kwenye kituo cha treni mjini Seoul, Korea Kusini, Septemba 28, 2022.

Korea Kaskazini imefanya jaribio lake la pili la makombora wiki hii saa kadhaa kabla ya makamu wa rais wa Marekani, Kamala Harris, kujiandaa kutembelea eneo huru linalo tenganisha Korea Kusini na Kaskazini.

Ilifanya majaribio ya makombora ya masafa mafupi Jumatano jioni kuelekea katika mwambao wa mashariki, jeshi la Korea Kusini limesema katika taarifa kwa wanahabari.

Serekali ya Japan pia imeripoti kufanyika kwa majaribio hayo lakini hakuna taarifa zaidi zilizo tolewa.

Majaribio hayo yamefanyika baada ya siku tatu toka Korea Kaskzini kujaribu makombora ya masafa mafupi.

Mpaka sasa imeshafyatua makombora 34 kwa mwaka huu kiwango ambacho ni cha juu.

Majaribio haya ya sasa yanachukuliwa kama vitisho toka maafisa wa Marekani kupanga ziara ya makamu wa rais wa Marekani kutembelea eneo huru maarufu kama DMZ.

XS
SM
MD
LG