Jaribio lililoshindikana la Korea Kaskazini kurusha kombora la masafa marefu leo Ijumaa inaonekana si kitu ambacho kitarudisha nyuma jeshi, wachambuzi wanasema.
Badala yake ni sehemu ya mafanikio ya kawaida katika maendeleo ya kuimarisha program ya silaha za nyuklia.
Kumekuwepo na ongezeko la wasi wasi juu Korea Kaskazini kuongeza uwezo wa makombora na nyuklia, wakati nchi hiyo inaendelea kutishia majirani zake, Korea Kusini na Japan pamoja na Marekani.
Inasadikiwa kwamba Korea Kaskazini haikufanikiwa kufanya jaribio la kombora la masafa ya kati la Musudan ambalo halijawahi kufanyiwa majaribio.