Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 17:02

Korea Kaskazini kuruhusu wananchi kufuatilia vyombo vya habari vya Korea Kaskazini


Korea Kusini imepanga kuondoa marufuku yake ya muda mrefu ya watu wake kutotazama televisheni za Korea Kaskazini, kusoma magazeti, na kufuatilia vyombo vingine vya habari.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za kuleta maelewano baina ya mataifa hayo pinzani maafisa wamesema Ijumaa, licha kuwepo kwa hali ya utata kutokana na majaribio ya makombora ya Korea Kaskzini ya hivi karibuni.

Yakitenganishwa na mpaka wenye uangalizi zaidi toka mwaka 1948, Korea hizo mbili ilikataza wananchi wake kutembeleana katika himaya zao, na kuwasiliana kwa njia ya simu, barua ama barua pepe, na zilizuia kupatikana kwa mitandao ikiwa pamoja na vituo vya Televisheni.

Katika ripoti ya sera hiyo kwa rais mpya wa Yoon Suk Yeol ya Ijumaa, wizara ya Korea ya kuleta muungano imesema kwamba kwa sasa itafungua milango kwa matangazo ya Korea Kaskzini.

XS
SM
MD
LG