Afisa wa pili kwa cheo cha juu katika ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Uingereza amekimbilia Korea Kusini kwa mujibu wa wizara ya muungano ya Korea Kusini.
Thae Yong Ho amewasili na familia yake katika mji mkuu wa Korea Kusini wa Seoul alisema msemaji wa wizara hiyo Jeong Joon Hee . Kwa sasa wako chini ya usimamizi na ulinzi wa serikali Jong aliwaambia waandishi wa habari.
Jeong alisema Thae aliwaambia maafisa wa Korea Kusini kwamba aliamua kuondoka kutokana na kukasirishwa na serikali ya Korea Kaskazini na kiongozi wake Kim Jong Un akitamani demokrasia iliyopo Korea kusini na wasi wasi juu ya siku zijazo za watoto wake.