Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:25

Korea Kusini yatazama muenendo wa Korea Kaskazini kwa makini


Serikali ya Korea Kusini leo haikudhibitisha ripoti za kuanza tena kwa uzalishaji wa madini ya Plutonium nchini Korea Kaskazini, lakini ikasema kwamba inatazama kwa makini miendo ya taifa hilo jirani.

Msemaji wa muungano wa kitaifa, Jeong Joon-Hee, aliwaambia waandishi wa habari kwamba ni jambo linalojulikana wazi kuwa Korea Kaskazini imekuwa ikijihusisha na shughuli nyingi ikitafuta uwezo wa kuongeza kiwango chake cha kemikali hiyo ya Plutonium.

Aliongeza kwamba Korea Kusini na Marekani zimeshirikiana kwa karibu kuhusiana na swala hilo.

Maafisa wa Marekani na wale wa Umoja wa Mataifa, ambao majina yao hayakutajwa, wanasema kwamba Korea Kaskazini inatumia tena mafuta ya kinyuklia ili kuzalisha madini ya Plutonium kwenye kituo chake cha YONGBYON.

XS
SM
MD
LG