Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 01:21

Korea kaskazini inasema Kim Jong Un anasimamia jaribio la ufyatuaji roketi


Kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong Un akitoa mwongozo wa ufyatuaji roketi katika picha isiyokuwa na tarehe ya tukio

Makombora yalisafiri kilomita zinazokadiriwa 220 kufikia urefu wa kilomita 25, ufyatuaji wake wa tatu wa aina hiyo katika muda wa zaidi ya wiki moja. Ripoti hiyo inatoka siku moja baada ya Korea kusini aliposema kaskazini ilifyatua makombora mawili kutoka jimbo la South Hamgyong

Korea kaskazini inasema kiongozi wao Kim Jong Un anasimamia jaribio la karibuni la ufyatuaji mfumo mpya wa roketi ambao unaripotiwa una uwezekano wa kuongeza uwezo wa Pyongyang kupiga malengo huko Korea kusini ikiwemo vituo vya jeshi la Marekani vilivyopo huko.

Shirika rasmi la habari la serikali ya Pyongyang limeripoti Jumamosi kwamba Kim alisimamia jaribio la mfumo mpya akitoa mwongozo wa ufyatuaji roketi kadhaa. Ripoti hiyo inatoka siku moja baada ya mkuu wa wafanyakazi huko Korea kusini aliposema kaskazini ilifyatua makombora mawili majira ya saa tisa alfajiri kwa saa za huko kutoka jimbo la South Hamgyong.

Makombora yalisafiri kilomita zinazokadiriwa 220 kufikia urefu wa kilomita 25, ufyatuaji wake wa tatu wa aina hiyo katika muda wa zaidi ya wiki moja.

Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong Un huko Panmunjom, Korea kusini, June 30, 2019.
Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong Un huko Panmunjom, Korea kusini, June 30, 2019.

Rais wa Marekani Donald Trump alipuuzia mzunguko mpya wa majaribio ya makombora ya Ijumaa ikiwa miezi mitano baada ya mazungumzo yake ya mwisho na kiongozi wa Korea kaskazini ya kudhibiti matumizi ya silaha za nyuklia na kuzusha ongezeko la shinikizo la namna ya kutafuta suluhisho la mkataba huo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG