Sung Kim amesema kwamba Korea kaskazini inapanga kufanya majaribio ya silaha za nuclear wakati wowote.
Maafisa wa ujasusi wa Korea kusini na Marekani, wamesema kwamba wamegundua juhudi za Korea kaskazini za maandalizi ya kufanyia majaribio silaha hizo hatari, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Endapo Korea kaskazini itatekeleza jaribio hilo, litakuwa la saba kufanyika tangu mwaka 2006.
Sung Kim, alikuwa akizungumza mjini Seoul, wakati wa mkutano na wawakilishi wa Korea kusini na Japan, ulioangazia vitisho vya Korea kaskazini vinavyoongezeka kutokana na mipango yake ya kutengeneza silaha za nuclear na makombora.
Mkurugenzi mkuu wa maswala ya Asia wa Japan, Funakoshi Takehiro, amesema kwamba misururu ya majaribio ya silaha za nuclear yaliyofaywa mwaka huu na uwezekano wa matayarisho ya majaribio yanaonyesha kuna haja yakujibiwa vikali na jumuiya ya kimataifa, na kulitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kuchukua hatua dhidi ya majaribio ya Korea kaskazini.
Facebook Forum