Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:27

Waandishi wazuia kuhudhuria halfa ya chama tawala cha Korea Kaskazini


TV zinaonyesha picha za kiongozi wa zamani wa Korea Kaskazini, marehemu Kim Jong Il na marehemu baba yake Kim Il Sung.
TV zinaonyesha picha za kiongozi wa zamani wa Korea Kaskazini, marehemu Kim Jong Il na marehemu baba yake Kim Il Sung.

Baada ya kuwaalika mamia ya wanahabari wa kimataifa kuripoti kuhusu chama kinachotawala kwa mara ya kwanza kwa muda wa miaka 36, Korea Kaskazini imewakataza wanahabari hao kuingia kwenye hafla hiyo.

Mkutano wa Worker's Party ' ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa kisiasa kufanyika Korea Kaskazini kwa vizazi kadhaa na unatarajiwa kuboresha nguvu ya kiongozi Kim Jong Un na kupitsha rasmi sera zake za "Byongjin" ili kusukuma mbele maendeleo ya kiuchumi na uwezo wa kinyuklia.

Mkutano wa mwisho kama huo ulifanyika mwaka wa 1980, kabla ya Kim Jong Un kuzaliwa, ambao ulimhalalisha baba yaka Kim Jong wa pili, kama mrithi wa Kim Il Sung, ambaye alikuwa babu yake kiongozi huyo wa sasa.

XS
SM
MD
LG