Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 17, 2025 Local time: 12:02

Kombora la Wahodhi lashambulia meli bahari ya Sham


Kombora lililoruswha na waasi wa Houthi wa Yemen, limepiga meli yenye usajili wa Liberia iliyokuwa ikisafiri kupitia Ghuba ya Aden, mamlaka zimesema Jumapili.

Hili ni shambulizi la kwanza la kundi hilo toka mashambulizi ya anga ya Israel kuanza kuwalenga.

Waasi Kihouthi hawakutoa maelezo kuhusu kusimamisha mashambulizi yao kwa wiki mbili dhidi ya meli zinazopita Bahari ya Shamu, ambayo yamepungua toka mashambulizi yalipoanza Novemba kwa sababu ya vita ya Israel na Hamas, Ukanda wa Gaza.

Kurejea kwa mashambulizi kumefanyika baada ya kuuawa kwa kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, nchini Iran, mfadhili mkuu wa Wahouthi, huku kukiwa na wasiwasi juu ya vita kuzuka katika mzozo huo wa kikanda.

Waasi hao wamesema waliiangusha ndege nyingine ya kijasusi ya Marekani Jumapili, na baadaye kuonesha picha za mabaki ya ndege hiyo kando ya mlima.

Forum

XS
SM
MD
LG