Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 04:52

Kombe la Dunia limeisaidia Qatar kuimarisha haki za wafanyakazi- Mratibu


Matangazo ya kombe la dunia ndani ya Mall ya Qatar REUTERS/Hamad I Mohammed.
Matangazo ya kombe la dunia ndani ya Mall ya Qatar REUTERS/Hamad I Mohammed.

Qatar inakubali kuwa kuna mapungufu katika mfumo wake wa ajira  lakini Kombe la Dunia limeruhusu nchi hiyo kupiga hatua katika masuala yanayohusiana na haki za wafanyakazi, Mahmoud Qutub, mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, alisema hivi karibuni.

Qatar inakubali kuwa kuna mapungufu katika mfumo wake wa ajira lakini Kombe la Dunia limeruhusu nchi hiyo kupiga hatua katika masuala yanayohusiana na haki za wafanyakazi, Mahmoud Qutub, mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, alisema Alhamisi.

Qatar, nchi ya kwanza ya Mashariki ya Kati kuandaa kombe la dunia imekuwa ikichunguzwa vikali na makundi ya haki za binadamu kuhusu jinsi inavyowatendea wafanyakazi wahamiaji katika maandalizi ya michuano hiyo, itakayoanza Novemba 20.

Licha ya juhudi za Qatar, Baraza la Ulaya lilisema matokeo zaidi yanahitajika kuonekana.

Idadi ya ajali mbaya inaendelea zinaendelea kuwakumba mamia. Na utekelezaji wa sheria mpya haufanyi kazi vizuri. “Wafanyakazi hawana haki ya kukusanyika," Bwana George Foulkes, ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho alisema.

Qutub, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati Kuu ya Ustawi wa Wafanyakazi na Haki za ajira, alisema kuwa hali ya wafanyakazi nchini Qatar imebadilika sana tangu FIFA ilipoipa fursa nchi hiyo ya mashariki ya kati kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2010.

“Tulianza safari hii baada ya kushinda zabuni ya Kombe la Dunia. Kulikuwa na kukiri wakati huo kwamba kuna mapungufu. Tumedhihirisha kupitia mifumo yetu mbalimbali ya ikolojia kwamba hatua za maana zinaweza kuchukuliwa ili kuziba mianya hiyo,” alisema.

Qutub alikuwa mmoja wa wazungumzaji katika kikao cha bunge cha umma kuhusu ulinzi wa haki za wafanyakazi nchini Qatar, kilichoandaliwa na Bunge la Baraza la Ulaya mjini Strasbourg.

XS
SM
MD
LG