Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:53

Koffi Olomide aachiwa kwa dhamana


Koffi Olomide akiwa na mkewe Aliya wakati alipokuwa kwenye gereza la Makala mjini Kinshasa.
Koffi Olomide akiwa na mkewe Aliya wakati alipokuwa kwenye gereza la Makala mjini Kinshasa.

Mwanamuziki wa rumba nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Koffi Olomide ameachiliwa kwa dhamana baada ya kukaa gerezani siku nne kwa kosa la kumpiga mmoja wa wacheza dansi wake.

Ijumaa mahakama ya Kinshasa ilitupilia mbali ombi la mawakili wa Olomide waliotaka aachiliwe kwa dhamana. Baadaye mahakama ya rufaa ilisikiliza hoja za mawakili na kutoa maamuzi ya kuachiliwa kwa dhamana.

Kwenye akaunti yake ya Twitter Olomide amewashukuru mashabiki wake. Pia amebandika picha ya mke wake Aliya na wanawe watatu, akiwemo Didi Stone Olomdie ambaye amesema "sioni tamko la ziada kuliko kusema ahsante kwa uungaji mkono wenu.. Ninayohisi ndani ya moyo wangu ni makubwa kuliko "merci" ahsante".

XS
SM
MD
LG