Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 13:49

Kliniki moja yasaidia wanawake wagumba nchini Zimbabwe


Ramani ya Zimbabwe
Ramani ya Zimbabwe

Sehemu kubwa barani Afrika,ikiwa ni pamoja na Zimbabwe, wanawake wanaohangaika kupata watoto mara nyingi wanakabiliwa na unyanyapaa na kejeli. Ili kusaidia kumaliza shida hiyo, madaktari wawili wa Zimbabwe mwaka 2017 walifungua tena kliniki ya kipekee nchini humo ya kusaidia uzazi kwa nia ya kupandikiza.

Tangu kliniki hiyo ilipofunguliwa tena mnamo mwaka 2017, miaka kadhaa baada ya mmiliki wake wa zamani kustaafu, IVF Zimbabwe inaelezewa imesaidia wanawake wapatao 120 kupata watoto kupitia virtubisho vya mbegu.

Madaktari Tinovimba Mhlanga na Sydney Farayi wanasema baadhi ya wanandoa wanahangaika kupata watoto kwa sababu ya ukosefu wa maarifa na fedha lakini wanafuraha kuwasaidia kufikia malengo yao.

Mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 30 anatarajia kujifungua mwezi ujao baada ya kupata msaada kutoka kwa IVF Zimbabwe katika ndoa yake ya pili. Ya kwanza ilivunjika baada ya miaka saba ya kutokuweza kupata uja uzito na hataki kutajwa jina.

Shirika la Umoja wa Mataifa linasema kushindwa kupata mimba barani Afrika kunalaumiwa sana kwa wanawake, ingawa nusu ya visa vya utasa husababishwa na changamoto ambazo wanaume wanakabiliwa navyo.

Shirika la Afya Ulimwenguni la Umoja wa Mataifa linasema changamoto za utasa ni za kawaida na zinaweza kumalizwa.Lakini barani Afrika, serikali nyingi mara nyingi huzingatia zaidi chamgamoto za kiafya kama magonjwa ya milipuko, magonjwa ya kuambukiza na utapiamlo.

Wagonjwa katika IVF Zimbabwe wanasema wanalipa karibu dola 4,000 kwa matibabu fedha nyingi sana kwa mtu wa kawaida nchini Zimbabwe.

Lakini kwa wateja walio tayari kumpokea mtoto wao wa kwanza baada ya kusubiri kwa muda mrefu, uwekezaji huo una thamani yake.

XS
SM
MD
LG