Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:47

Kiwango cha joto kuongezeka zaidi ya mara 30


Watu wasiokuwa na makao wakiwa wamelala chini ya barabara ya juu mjini New Delhi, India, kutokana na kiwangio cha juu cha joto.
Watu wasiokuwa na makao wakiwa wamelala chini ya barabara ya juu mjini New Delhi, India, kutokana na kiwangio cha juu cha joto.

Wanasayansi wa kimataifa wamesema kwamba joto lililozikumba India na Pakistan katika miezi ya hivi karibuni, lilisababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na kwamba linaashiria namna hali itakavyokuwa katika siku za baadaye.

Kundi la watabiri wa hali ya hewa duniani, limesema kwamba mabadiliko ya hali ya hewa ya sasa yanasababishwa na biandamu, na kupelekea viwango vya joto kuongezeka kwa zaidi ya mara 30.

Wamesema kwamba iwapo kiwango cha joto kitaongezeka kwa nyuzi joto 2, hali ya joto la joto linaweza kujitokeza mara moja kila baada ya miaka mitano.

XS
SM
MD
LG