Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 13:01

Kituo cha kusafirisha mafuta cha Nigeria kilikuwa na njia ya wizi baharini kwa miaka 9


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Maafisa nchini Nigeria waligundua njia haramu ya kuunganisha mafuta kutoka kwenye  mojawapo ya njia yake kuu ya kusafirisha mafuta baharini ambayo imekuwa ikifanya kazi bila kutambuliwa kwa miaka tisa, mkuu wa kampuni ya mafuta ya serikali NNPC LTD alisema.

Bomba hilo linalounganisha kilomita 4 kutoka kwenye kituo cha usafirishaji cha Forcados, ambacho kwa kawaida husafirisha takriban mapipa 250,000 kwa siku ya mafuta, ndani ya bahari ilipatikana wakati wa kuzuia wizi katika wiki sita zilizopita, Mkuu wa NNPC Mele Kyari aliambia kamati ya bunge jumanne usiku.

Wizi wa mafuta nchini humo umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miaka 22 lakini kiwango ambacho kilidhaniwa katika siku za hivi karibuni hakijawahi kutokea, Kyari alisema katika mahojiano kutoka kwenye mkutano huo yaliopatikana na Reuters.

Mara nyingi wezi hupasua mabomba ya ardhini ili kunyonya mafuta bila kutambuliwa wakati wanaendelea kufanya kazi, lakini njia isiyo halali baharini si ya kawaida sana na inapendekeza operesheni ya wizi wa hali ya juu zaidi.

XS
SM
MD
LG