Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:06

Kenya yaunganisha idara za usalama kupambana na Ugaidi


Joseph Nkaissery
Joseph Nkaissery

Kituo kimoja chenye kusimamia vyombo vya usalama mbalimbali nchini Kenya kimeanzishwa ilikukabiliana na mashambulizi ya kigaidi na matukio ya uvunjifu wa amani wakati wa kipindi cha uchaguzi.

Kikundi cha maafisa 530 waliochukuliwa kutoka katika Usalama wa Taifa (NIS), Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), Jeshi la Polisi la Taifa (NPS), Huduma za Mapori Kenya (KFS), Jeshi la Magereza, Kikosi cha Wanyama pori (KWS) na Huduma ya Vijana ya Taifa (NYS) watafanya kazi kwa pamoja na kushirikiana katika kuratibu njia bora ya kukabiliana na masuala ya uvunjifu wa amani wakati wa kipindi cha uchaguzi.

Kitengo cha operesheni za Maafa cha Taifa, Kikosi cha Zimamoto, makamishna wa kaunti zote na Huduma ya gari ya wagonjwa ya St Johnsitakuwa ni sehemu ya watakaoshiriki katika mafunzo ambayo yamepewa jian la zoezi la kudumisha utulivu.

Zoezi hilo linakusudio la kuzuia matukio ambayo yatapelekea vyombo vya usalama kufanya kazi bila ya kushirikiana pamoja kitu ambacho kinaweza kupelekea kuleta vurugu na mapungufu ya kiutendaji kama ilivyowahi kutokea wakati wa shambulizi la kigaidi lililotokea Westgate na Chuo Kikuu cha Garisaa.

Vyanzo vya habari nchini Kenya vimesema kuwa mratibu wa zoezi hili ni Waziri wa Mambo ya Ndani Joseph Nkaissery, ambaye amekabidhiwa jukumu la kuhakikisha nchi haitumbukii katika jamba la machafuko kama yaliyowahi kutokea 2007/2008.

"Tunataka kuhakikisha nchi yetu inabakia kuwa na amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Tutahakikisha tunaushirikiano wa kutosha kati ya vyombo vya usalama na wadau wote nchini," Nkaissery amesema.

XS
SM
MD
LG